Monday, 1 February 2016

AJIRA HATARISHI KWA WATOTO

ad300
Advertisement

Katika mazingira yetu ya Kitanzania na bara la Afrika kwa ujumla kumekuwa na  ukiukwaji kubwa sana wa HAKI ZA WATOTO katika swala zima la ajira licha ya kuwepo kwa  sheria mbalimbali hususani SHERIA YA AJIRA NA MAHUSINO KAZINI. Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini hii ni sheria nambari nane (8) ya mwaka 2006, sura ya (366).

Wanajamii wengi wamekuwa wakitenda makosa mbalimbali kwa kutojua ama kwa kujua sheria, hususani sheria ya ajira na mahusiano kazini inasema nini  kwa watoto. Embu tuitazame kwa makini sheria hii. 

  

[ 20.Disemba.2007] [T.S.N na.1 ya 2007]

SEHEMU YA II HAKI ZA MSINGI NA ULINZI.

 Sehemu Ndogo A – Ajira kwa Watoto 

5.-(1) Hakuna mtu anayeruhusiwa kumuajiri mtoto mwenye umri chini ya miaka kumi na nne.

     (2) Mtoto mwenye umri wa miaka kumi na nne anaweza kuajiriwa kufanya kazi nyepesi tu, ambazo haziwezi kuwa na madhara kwa afya ya mtoto na maendelo yake; na hazimzuii mtoto kuhudhuria masomo shuleni, kushiriki kwenye ufundi stadi au miradi ya mafunzo iliyothibitishwa na mamlaka yenye madaraka au uwezo wa mtoto kufaidi maelekezo anayoyapata. 

     (3) Mtoto mwenye umri chini ya miaka kumi na nane haruhusiwi kuajiriwa kwenye mgodi, kiwanda au kama kufanya kazi katika meli au katika sehemu nyingine za kazi ikijumuisha ajira isiyo maalumu na kilimo, kwenye mazingira ya kazi ambayo Waziri anaweza kuona ni hatarishi. Kwa madhumuni ya kifungu kidogo hiki, “meli” inajumuisha chombo cha aina yoyote kinachotumika kwa usafiri wa maji.  

    (4) Mtu yeyote haruhusiwi kumwajiri mtoto kwenye ajira- 

     (a) ambayo haifai kwa mtu mwenye umri huo;

      (b) sehemu ambayo inayohatarisha hali nzuri ya mtoto, elimu, afya ya mwili na akili, au roho, maadili au maendeleo ya kijamii. 

      (5) Bila kujali masharti ya kifungu kidogo cha (3), sheria yoyote ile iliyoandikwa inayoratibu masharti ya mafunzo inaweza kuruhusu mtoto mwenye umri wa chini ya miaka kumi na nane kufanya kazi- 

    (a) katika meli ya mafunzo kama sehemu ya mafunzo ya mtoto; 

     (b) (c) katika kiwanda au mgodi kama kazi hiyo ni sehemu ya mafunzo ya mtoto; katika sehemu nyingine ya kazi kwa masharti kwamba afya, usalama na maadili ya mtoto yanalindwa ipasavyo na kwamba mtoto amepokea au anapokea maelekezo maalumu ya kutosha au mafunzo ya ufundi katika kazi au shughuli inayohusika.

   (6) Waziri anaweza kutengeneza kanuni-

         (a) kuzuia, au kuweka masharti katika ajira ya watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane; 

         (b) kuamua muundo wa kazi zilizotajwa katika kifungu kidogo cha (4) cha Sheria hii na kuweka masharti ya mapitio ya mara kwa mara na kuiboresha orodha ya mfumo wa kazi za hatari.

    (7) Ni kosa kwa mtu yeyote-

        (a) kumuajiri mtoto kwa kukiuka hiki kifungu; 

        (b) kumshawishi mtoto kuingia kwenye ajira kwa kukiuka kifungu hiki.

     (8) Katika mwenendo wowote chini ya kifungu hiki, kama umri wa mtoto unabishaniwa, kazi ya kuthibitisha kwamba ilitosha kuamini, baada ya uchunguzi, kwamba mtoto hakuwa mwenye umri wa chini kwa madhumuni ya kifungu hiki itakuwa kwa mtu anayemwajiri au anayemshawishi mtoto kuingia kwenye ajira. 

 Sehemu Ndogo B – Kazi ya Lazima Kuzuia ajira chini ya usimamizi na udhibiti wa mamlaka ya umma na kwamba mtu huyo hajaajiriwa au hajawekwa kwenye mikono ya watu binafsi; kazi yoyote inayotolewa katika hali ya hatari au mazingira ambayo yatahatarisha uwepo au maisha mazuri ya jamii yote au sehemu ya jamii; huduma ndogo za jamii zinazofanywa na wanajamii kwa maslahi yao ya moja kwa moja baada ya kushauriana nao au wawakilishi wao juu ya umuhimu wa huduma. 

 Sehemu Ndogo C: Ubaguzi

       7.-(1) Kila mwajiri atatakiwa kuhakikisha kwamba anaendeleza fursa sawa katika ajira na kujitahidi kuondoa ubaguzi katika sera yoyote ya ajira mazoezi kwa vitendo. 

           (2) Mwajiri atalazimika kusajili kwa Kaminishna wa Kazi, mpango wa kuendeleza fursa sawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi. 

           (3) Kamishna wa Kazi anaweza kumtaka mwajiri

       (a) kutayarisha mpango uliotajwa katika kifungu kidogo cha 

       (2); na (b) kusajili huo mpango kwa Kamishna. 

           (4) Mwajiri yeyote asifanye ubaguzi wa dhahiri au usiokuwa wa dhahiri kwa mwajiriwa, katika sera au mazoea katika moja ya sababu zifuatazo:

         (a) rangi;

         (b) utaifa; 

         (c) kabila au sehemu anayotoka; 

         (d) asili 

         (e) Uasili wa Taifa;

         (f) asili ya kijamii; 

         (g) maoni ya kisiasa au kidini; 

         (h) Mwanamke au Mwanaume;

         (i) jinsia;

          (j) ujauzito; 

          (k) kuolewa au kutoolewa au majukumu                            ya familia; 

         (l)ulemavu; 

         (m)VVU/UKIMWI; 

          (n) Umri; au 

          (o) maisha anayoishi. a kulazimishwa Sura ya 192 

     6.-(1) Mtu yeyote anayeshawishi, anayehitaji au anayetoa kazi ya lazima, anatenda kosa. 

          (2) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, kazi ya lazima inajumuisha kazi ya utumwa au kazi yoyote iliyolazimishwa kwa mtu kwa vitisho vya adhabu na ambayo mtu huyo hajaridhika lakini haijumuishi -

          (a) kazi yoyote inayotolewa chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taifa ya mwaka 1966, kwa kazi ambayo ni ya kijeshi; 

          (b) (c) kazi yoyote ambayo ni sehemu ya wajibu wa kawaida wa kiraia kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; kazi yoyote inayotolewa kwa mtu yeyote ikiwa ni matokeo ya kutiwa hatiani na mahakama ya sheria, ikiwa inafanyika. 

Hivyo basi kutoka na sheria hii imeweka baadhi ya mambo bayana na kwa uwazi wanajamii hatuna budi kutii sheria hii bila shuruti pamoja na Serikali na wadau mbalimbali wa watoto tutoe Elimu kwa jamii ili kuweza kuhakikisha maslahi bora ya watoto nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla yanafikiwa kwa kasi  ili kuweza kuakikisha watoto wanakuwa salama na wana kuwa wazalendo katika nchi yao.Nakwenda sambamba na wale wote wanaokiuka  sheria kwa kuwa wakandamiza watoto,ili tuweze kufikia lengo kuu na kuyatekeleza kwa usahihi na kufikia Malengo Endelevu pindi ifikapo mwaka 2030.

             "WATOTO DARAJA BORA KATIKA JAMII" 


Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: