Advertisement |
Kwa muda wa miongo mingi sasa taasisi za kiraia pamoja na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yamekuwa na mchango mkubwa sana licha ya changamoto zake katika jamii zetu hususani jamii za kiafrika.
Swala zima la utoaji wa elimu ya uraia mashuleni linabudi kuendelezwa mbele kwani kwa kipindi hiki linaonekana kufifia sana.
Jamii hususani Wazazi na Walezi wamekuwa wakiwanyooshea watoto wao vidole kwa kusema watoto wa siku hizi hawana maadili mema kama ilivyo kuwa nyakati zao. Hili laweza kuwa na ukweli ndani yake. Kama lina ukweli ndani yake basi yatupasa tutambue sisi kama wanajamii wapi tulipo kosea ili tuweza kutatua tatizo hili kwani tuna amini huwezi kutatua tatizo kwa asilimia kubwa bila kujua visababishi vya tatizo hilo.Kama tatizo ni utandawazi basi kuna umuhimu mkubwa kuwafundisha watoto wetu namna ya kuendana vyema na utandawazi kwani utandawazi kwa zama hizi haukwepeki ingawa una madhara makubwa ukitumika vibaya hivyo watoto wapaswa kujua na kuacha kutumia vibaya utandawazi.
Kwa kipindi cha zama hizi watoto wengi huwa maeneo ya shuleni tofauti na zama za nyuma kidogo ambopo idadi kubwa ya watoto hawakuweza kupata fursa ya kwenda shule. Hivyo mashirika yasiyo ya kiserikali yakishirikiana pamoja na serikali yameamuua kujikita zaidi katika utoaji wa ELIMU YA URAIA mashuleni kama lifanyavyo SISI NA WATOTO ili kuakisha linajenga msingi mzuri kwa kizazi cha sasa na kijacho kwani SISI NA WATOTO tunaamini katika kauli mbiu yetu "WATOTO DARAJA BORA KATIKA JAMII" hivyo hatuvuki daraja hili bila kuakikisha linakua bora kwa manufaa ya Jamii yetu ya kitanzania na dunia kiujumla. Wanajamii yatupasa tuungane kwa pamoja kuleta mabadiliko chanya katika maswala mbalimbali ya Watoto.
"WATOTO DARAJA BORA KATIKA JAMII "
0 comments: