Advertisement |
1.Utangulizi
Kabla ya kutungwa kwa Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 maswala ya mtoto nchini Tanzania yalikuwa yameunganishwa katika Sheria ya Malezi,(Sura ya 278),Sheria ya kuasili Mtoto(Sura ya 335), Sheria ya Udhibiti wa Nyumba za Watoto (Sura ya 61), na Sheria nyingine. Hali hii ilisababisha ugumu katika uelimishaji na utekelezaji wa masharti husika.
Mnamo mwaka 2009 Serikali iliamua kutunga Sheria mpya ya Mtoto kwa lengo la kuunganisha masharti husika katika sheria moja na kuyaboresha zaidi kulingana na mazingira yetu.
Hali halisi ya kijamii na kiuchumi pamoja na Mikataba ya kimataifa ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini na kuridhia ikiwemo Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto, pamoja na hitifaki zake za nyongeza na Mkataba wa Haki na Ustawi wa Mtoto wa Afrika.
Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 4 Novemba,2009 na kusainiwa na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (mstaafu awamu ya nne) tarehe 20 Novemba,2009.
Sheria hii imechapishwa katika gazeti la Serikali Namba 156 na kuanza kutekelezwa tarehe 16 Aprili,2010.
2.Madhumuni
Sheria ya Mtoto Na.21 ya mwaka 2009 ina madhumuni yafuatayo:-
1. Kurekebisha na kuweka pamoja masuala ya mtoto katika sheria moja ya Mtoto.
2. Kuweka masharti maalum kwa ajili ya kuendeleza ,kuboresha,kuhifadhi na kulinda Haki za Mtoto zilizoainishwa katika sheria mbalimbali ili kukidhi matakwa ya Mikataba ya Kimataifa na Kikanda kuhusu Haki na Ustawi wa mtoto tuliyoisaini na kuridhia. Hii ni pamoja na Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008.
3. Kuweka masharti yanayoondoa ubaguzi kwa mtoto pamoja na ubaguzi wa kijinsia, dini, ulemavu na Siasa.
4. Kulinda na kuhifadhi haki za mtoto na kutoa tafsiri ya neno "Mtoto" ambalo litatumika sambamba na tafsiri katika Sheria zote za nchini, Katiba ya Nchi, Mikataba ya Kimataifa na sera ya Taifa ya Maendeleo ya mtoto ya mwaka 2008.
5. Kuanisha Haki za mtoto kwa kuzingatia misingi ya Ustawi, haki ya Kuishi na wazazi wake, kudhibiti vitendo vitokanavyo na mila zinazoleta madhara ,kuzuia na kudhibiti ajira hatarishi kwa watoto kwa kuzingatia watoto wenye mahitaji maalum.
6. Kuweka mazingira yatakayoongoza taratibu za matunzo kwa mtoto kwa kuzingatia gharama za maisha , sehemu husika na hali halisi ya kiuchumi pamoja na uwezo wa wazazi.
7. Kuweka masharti yanayohusu watoto walio katika ukinzani na sheria kwa kuainisha utaratibu wa kumshughulikia mtoto na kutoa adhabu mbadala ya kifungo kwa lengo la kumrekebisha na kuweka masharti ya kuasili mtoto.
0 comments: