Advertisement |
Ugumu wa maisha kwa Watanzania walio wengi unapelekea moja kwa moja kwa watoto kutoweza kuendelea na elimu na kujingiza katika shughuri za kutafuta pesa ili waweze kuinua familia zao kwani baadhi yao wanashika nafasi ya mzazi ndani ya familia kama vile kulea wadogo zao wangali wao binafsi ni wadogo na wanahitaji malezi ya karibu kabisa kutoka kwa wazazi/walezi wao ili waweze kukua vyema. Jamii pamoja na Serikali yapaswa kutengeneza mazingira yaliyo bora zaidi pamoja na kutekeleza kwa kina mipango yake na mikakati kabambe zaidi ya kuondoa umaskini, na kuwezesha watoto wanaojihusisha na shughuri zisizo maalumu ama hatarishi waweze kujengewa mazingira ya kupata elimu ya ufundi,biashara,sanaa na kujenga zaidi shule vitakazo weza kukuza na kuendeleza vipaji kwa watoto kwani watoto wamejaliwa vipawa vikubwa, hivyo jamii na serikali haina budi kuweka mikakati kabambe itakayotekelezeka na kuendeleza maslahi bora kwa mtoto.
0 comments: