Thursday 7 April 2016

Mauaji ya Kimbari yalivyo waathiri watoto nchini Rwanda

ad300
Advertisement

Mauaji ya Kimbari ya Rwanda yalikuwa mauaji ya halaiki nchini Rwanda mnamo mwaka wa 1994 ambapo Watutsi, Watwa na baadhi ya watu wa kabila la Kihutu waliuliwa na serikali iliyosimamiwa na viongozi wa Kihutu.

Katika kipindi cha takriban siku 100, kuanzia kuuliwa kwa Habyarimana na Ntaryamira tarehe 6 Aprili hadi katikati mwa mwezi Julai, walau watu 500,000 waliuawa, au karibu asilimia 20% ya idadi ya watu nchini Rwanda wakati huo.

Kuuawa Habyarimana tarehe 6 Aprili 1994 kulikuwa chanzo muhimu cha mauaji ya kimbari nchini humo. Kuhusiana na kuuawa Habyarimana, Wahutu wenye misimamo ya kufurutu mpaka walihusisha tukio la kutunguliwa ndege yake na wapinzani wa Kitutsi na kulitumia kama kisingizio cha kuanzishia mashambulio na mauaji makubwa na ya kutisha dhidi ya Watutsi, Watwa na Wahutu wenye misimamo ya wastani.

Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yaliendelea kwa muda wa siku 100 hadi hali ya mambo ilipodhibitiwa na vikosi vya waasi wa wakati huo wa RPF, wapiganaji wake wengi wakiwa ni Watutsi.

Inasemekana kuwa watu wapatao laki nane waliuawa, wengi wao wakiwa Watutsi, lakini wakiwemo pia Wahutu wenye misimamo ya wastani.

Mauaji hayo ya Kimbari yaliwaacha watoto wengi sana katika hali ngumu mno wengi wao wakiwa wamebaki yatima na wengi kuathirika kisaikolojia kutokana na vitendo vya kinyama vilivyokuwa vikitendeka mbele yao.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: