Advertisement |
Leo ni madhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.
Wanawake duniani wanaadhimisha madhimisho hayo huku wakiwa wanakabiriwa na matatizo mbalimbali hususani ya kijinsia kama vile udhalishaji wa kingono, ukeketeji pamoja na ukosefu wa usawa katika jamii baina yao na wanaume husasani katika maswala ya kielimu na uwajibikaji katika shughuli za kila siku zinazofanyika kila siku ndani ya jamii.
Hivyo Jamii pamoja na Serikali zinaitajika kuungana kwa pamoja ili kutatua changamoto zinazowakabili Wanawake duniani kote hususani barani Afrika.
Elimu ya kutosha ndo nguzo imara ya kutatua na kumaliza kabisa matatizo yanawakabili wanawake pamoja na makundi maalumu ndani ya jamii kama vile watoto na watu wenye ulemavu.
Ushirikiano pia ni nguzo muhimu katika kutatua matatizo yanayowakabili wanawake.
Vyombo vya usalama kama vile jeshi la Polisi hazina budi kushirikiana bega kwa bega na mihimili ya dola. Mahakama pamoja na Bunge zinabudi kusimamia sheria vyema hili kuakikisha Wanawake na makundi yote yanapata haki zao.
#sikuyawanawakedunianimarch8 #sisinawatoto
0 comments: