Advertisement |
Ugonjwa wa Usonji kwa lugha ya kiingereza ni Autism, ni ugonjwa ambao kwa mujibu wa shirika la afya duniani, WHO hukumba mtoto mmoja kati ya kila watoto 160 duniani. Usonji ni tatizo la kibaiolojia analopata mtoto anapokuwa tumboni mwa mama yake na dalili huonekana kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea.Kabla ya hapo wataalamu wanasema ni aghalabu kuona dalili hizo ambapo zinapojitokeza mtoto hukosa mbinu za uhusiano, anashindwa kuzungumza na wakati mwingine kurukaruka na hata kujing'ata. Watoto hawa kutokana na tatizo hilo wengine hutekelezwa na jamii na kunyimwa haki zao za msingi ikiwemo kuishi, kuendelezwa, kulindwa na kushirikishwa. Hata hivyo katika siku ya kimataifa ya usonji duniani tarehe Pili Aprili Umoja wa Mataifa umetaka elimu zaidi ili jamii ibadili mtazamo kwani watoto wenye usonji wakipatiwa huduma mapema wanaweza kushiriki vyema katika jamii zao kwani wana uelewa wa hali ya juu. Nchini Tanzania harakati za kuelimisha jamii kuhusu Usonji zilikwishaanza.
#Sambaza #share #autism #usonji #tanzania #sdgs
0 comments: