Advertisement |
September 26th, 2016 Watoto kutoka katika viunga mbalimbali vinavyounda Halmashauri ya Wilaya ya Moshi walikusanyika kwa pamoja katika Ofisi za Halmashauri hiyo maarufu kama "KDS" kuwawakilisha watoto wenzao ambao hawakuweza kupata fursa hiyo.
Lengo na dhumuni la mkutano huo ilikuwa ni Uchaguzi Mkuu wa kupata baraza jipya la Watoto Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kama ulivyo utaratibu wa mabaraza ya Watoto nchini Tanzania uchaguzi Mkuu wa Mabaraza ya Watoto hufanyika kila baada ya miaka miwili, wale ambao umri wa miaka 18 hawataruhusiwa tena kugombea nafasi yoyote ndani ya Baraza hilo hila baadhi ya viongozi waliovuka umri wa miaka 18 wanapata nafasi ya kuwa Washauri wa Baraza husika,kama ilivyofanyika kwa Baraza la Watoto Halmashauri ya Wilaya Moshi Mwenyekiti ambae amemaliza muda wake ndg Mohamed R. Gea na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo ndg Peniel Mlay watakuwa washauri wa Baraza hilo ambalo litaongozwa chini ya Mwenyekiti mpya ndg Kingslay Sama.
Baraza la Watoto ni chombo huru kilichoundwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Watanzania ili kiwezesha maslahi bora ya mtoto nchini yanalindwa na watoto wenyewe wanapata nafasi ama chombo cha kuwawakilisha.
Kauli Mbiu ya Baraza la watoto ni:- "KULINDA NA KUTETEA HAKI ZA MTOTO NI JUKUMU LANGU MIMI NA WEWE"
0 comments: