Advertisement |
HISTORIA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA.
Historia;
Katika bara la Afrika nchi nyingi sana zilikuwa zikitawaliwa na Wakoloni isipokuwa nchi mbili tu barani Afrika ambazo hazi kutawaliwa nazo ni Ethiopia na Liberia.
Nchi ya Afrika Kusini(South Afrika) ndio ilikuwa ya mwisho barani Afrika kujipatia Uhuru wake kutoka kwa Wakoloni, ilijipatia Uhuru wake mnamo mwaka 1994, ambako Afrika Kusini ilikuwa chini ya Utawala wa Makaburu kwa kipindi cha muda mrefu.
Katika Utawala wa Makaburu ubaguzi kwa Waafrika ulifanyika kwa kiwango kikubwa hususani ubaguzi wa rangi baina ya wazungu na Waafrika, ubaguzi ulifanyika katika nyanja mbalimbali za kijamii,uchumi na siasa na viliongozwa na kutekelezwa kwa hali ya juu na serikali ya Makaburu ili kuweza kuakikisha mwafrika anakuwa chini kimaendeleo.
Ili kuweza kakikisha Mwafrika anakuwa chini serikali ya Makaburu ilijiwekea mikakati ya ukandamizaji katika nyanja zote za maendeleo.
Mnamo mwaka wa 1953 serikali ya makaburu ilianzisha sheria ya elimu ya Wabantu iliyojulikana kama "THE BANTU EDUCATION ACT" ambayo moja kwa moja ilipelekea kuanzishwa kwa idara ya elimu ya elimu ya Afrika iliyojulikana kama "BLACK EDUCATION DEPARTMENT" iliyokuwa chini ya Wizara ya Mambo ya Wazawa (Ministry of Native Affairs) shughuli kubwa ya Wizara hiyo ilikuwa ni kutenganisha mfumo wa elimu kati ya watoto wa kizungu na watoto wau kiafrika na kuandaa mitaala ya elimu ambayo walihisi inaendana na Waafrika!!!.
Katika mfumo huu wa elimu watoto Waafrika walihitajika kulipa ada kwa ajili ya shule na michango mingine ya elimu, huku ikiwa kinyume kabisa na na watoto wakizungu ambao walisoma bure na kupata mahitaji muhimu ya shule kama vile vitabu,madaftari na kalamu bila kulipia michango yoyote ya kifedha ama chochote kitu. Waziri wa Mambo ya Wazawa wa wakati huuo "Hendrik Verwoerd aliwahi kusema " Wazawa lazima wafundishwe kuanzia hatua za mwanzo kabisa kuwa Waafrika hawawezi wakawa sawa na wazunguna mwafrika hatopatiwa elimu elimu itakayo muwezesha kupata cheo katika jamii badala yake watapewa ujuzi utakao wawezesha kuhudumia majumbani kwao na kufanya kazi chini ya wazungu". !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!π
Shule nyingi mjini SOWETO (South and Western Townships) zilikuwa hazina zana za kufundishia, walimu wachache na wasio kidhi sifa ufundishaji, katika shule za aina hizo ndo watoto wakiafrika walisoma huku wakiwa wanafunzi wengi na madarasa yakiwa machache kuliko idadi ya wanafunzi.
Chini ya serikali ya Makaburu na mfumo wake huu wa elimu hakuna shule mpya iliyowahi kujengwa tangu mwaka1961-1971.
Mnamo mwaka 1974 idara ya elimu ya Waafrika chini ya makaburu ili tangaza rasmi kuwa lugha ya kiafrikana ndio lugha ndio itakayo kuwa lugha maalumu ya kufundishia wanafunzi wa Kiafrika kuanzia darasa la tano na kuendelea, huku watoto wa kizungu wakiendelea kufundishwa kwa lunga ya kiingereza, agizo ambalo lilitolewa bila hata kuwashirikisha Waafrika ambao ndio wahusika.
Lugha ya kiafrikana ni lugha ndogo ambayo ilikuwa inachukua sehemu ndogo na ilizungumzwa na watu wachache sana wengi wa walimu nao walikuwa hawawezi kufundisha kwa kutumia kiafrikana.
Kulikuwa na chama cha walimu wa kiafrika kilicho jukikana kwa jina la "THE AFRICAN TEACHERS ASSOCIATION" (ATASA) kiliweza kuanzisha kampeni ya kupinga agizo hilo.
Wanafunzi wa kiafrika hawakuwa tayari kuunga mkono agizo hilo kwa pamoja wakaamua kianzisha harakati za kupinga agizo hilo.
Mnamo mwaka 1976 walimu waligoma kufundisha kwa lugha ya kiafrikana.
Siku ya JUMATANO 16/06/1976 kati ya wanafunzi 15,000 hadi 20,000 walikusanyika katika maeneo mbalimbali ya mji wa SOWETO nchini Afrika Kusini wakiandamana kuelekea shule ya Sekondari itwayo ORLANDO WEST ambako wanafunzi wote walikubaliana kukutana ili kutangaza nia yao ya kupinga kufundishwa kwa kutumia lugha ya kiafrikana na mfumo wa elimu pamoja na sera ambazo ni baguzi kwao na zinazo wadidimiza kielimu.
Ndipo polisi walifika katika kilele cha maandamano hayo na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi sambamba na kuwasakizia mbwa na kuwaua kwa risasi. Hector Peterson(13) alikuwa wa kwanza kuuawa katika mashambulio hayo.
Zaidi ya watoto 100 waliuawa huku pia zaidi ya watoto 1000 walijeruhiwa.
Umoja wa nchi huru za Afrika,(OAU-Organisation of African Unity) kwa wakati huo kwa sasa (AU-African Unity) ilitambua na kuzingatia ushujaa madhubuti uliofanywa na wanafunzi hao,hivyo tarehe 16/06/1991 ikanzisha rasmi kuwa siku ya madhumisho ya mtoto wa Afrika, ambayo itakuwa itakuwa ina adhimishwa kila mwaka tarehe 16/06.
Siku ya Mtoto wa Afrika imewekwa kwa malengo ya kuendelea kutoa elimu bora kwa watoto waafrika sambamba na kupinga vitendo vyote vya ukiukwaji wa Haki za watoto.
Hivyo tuna budi kushirikiana kwa pamoja kuakikisha ustawi wa mtoto una kuwa bora zaidi barani Afrika.
MOHAMED RASHID GEA.
-Mshauri Baraza Watoto Tanzania.
-Mwenyekiti Baraza Watoto Halmashauri ya Wilaya ya Moshi.
-Founder Sisi na Watoto Social Group
Blog: sisinawatoto.blogspot.com
"CHILDREN ARE BETTER BRIDGE IN OUR COMMUNITY".
π«π©βπ©βπ¦βπ¦π―πΆππ½π¬π«π¬ππ¨ββ€οΈβπ¨πΌπΌπ©ββ€οΈβπ©ππ«π¬ππππ©ββ€οΈβπ©π©ββ€οΈβπ©π©ββ€οΈβπ©π«π―π¬π¬π¬π π¨ββ€οΈβπ¨ππ©ββ€οΈβπβπ©ππππππ¨ββ€οΈβπ¨π¨ββ€οΈβπ¨π¨ββ€οΈβπ¨ππππππ
#HAPPY MTOTO AFRIKA.
#HAPPY MTOTO AFRIKA.
#SISI NA WATOTO
0 comments: