Advertisement |
Baraza la Watoto Wilaya ya Lindi limefanya Uchaguzi katika ukumbi Chamikumbi Mkoani Lindi wa kuwapata Viongozi wapya kwa awamu nyingine watakao ongoza Baraza hilo kwa kipindi cha miaka miwili pamoja na kuzingatia jinsi na sifa za kuwa mwanachama (Kiongozi) katika nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Mwekahazina pamoja na Wajumbe kama ilivyo ainishwa katika Katiba ya Baraza la Watoto Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha tano-UANACHAMA NA JINSI YA KUJIUNGA.
5.1.2 Aina za uanachama: Baraza litakuwa na wanachama wa aina tatu (3) ambao ni:- a. Wanachama waanzilishi b. Wanachama wa Kawaida c. Wanachama wa kushirikishwa 5.1.3 Mwanachama mwaanzilishi ni mtoto yeyote mwenye umri usiozidi miaka kumi na na nane (18) ambaye ameshiriki katika mchakato wa kuunda na kusajili Baraza. 5.1.4 Mwanachama wa kawaida ni mtoto yeyote mwenye umri usiozidi miaka kumi na na nane (18)ambaye atajiunga na Baraza baada ya kusajiliwa kwa mujibu wa utaratibu wa kujiunga uanachama ambao utakuwa umewekwa na Katiba hii. 5.1.5 Mwanachama wa kushirikishwa ni mtoto yeyote mwenye umri usiozidi miaka kumi na na nane (18) ambaye atajiunga na Baraza lakini si raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na atakuwa na haki zote isipokuwa tu kupiga kura au kuchaguliwa kuwa kiongozi. 5.2 JINSI YA KUJIUNGA 5.2.1 5.2.2 Fomu ya maombi: Mtoto yeyote mwenye sifa za kujiunga kuwa mwanachama wa Baraza atajaza fomu maalum ya maombi ya uanachama na kuwasilisha kwa Katbu wa Baraza katika ngazi ya Klabu, Kata au Shehia, Wilaya au Mkoa. Kujadiliwa ombi la uanachama na Kamati ya Wilaya au Mkoa na Mkutano Mkuu: Kamati ya Wilaya au Mkoa itajadili na kutoa mapendekezo ya ama kukubali kumwingiza au kumkatalia uanachama mwombaji yeyote kutokana na kutimiza au kutotimiza sifa za uanachama. Mapendekezo ya Kamati yatawasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Wilaya au Mkoa na kisha kuwasilisha taarifa ya wanachama wapya kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Baraza ambayo itawasilisha orodha ya wanachama wapya kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la Watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 5.3 SIFA ZA UANACHAMA Mtoto yeyote mwenye umri usiozidi miaka kumi na nane ambaye anaishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anazo sifa za kuomba kuwa mwanachama wa Baraza. Isipokuwa ieleweke wazi kuwa mtoto asiye raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayo haki ya kuwa tu mwanachama mshiriki na kamwe si mwanachama wa Katiba ya Baraza la Watoto kawaida.
0 comments: