Advertisement |
Mzazi akiwa pamoja na mtoto wake wakiakikisha kulia na kushoto kama kuna usalama kisha waweze kuvuka barabara.
Ni vyema kuwafundisha watoto wetu elimu ya usalama barabarani kwani tutasaidia kupunguza ama kumaliza kabisa ajali za barabarani pindi wavukapo barabara.
Serikaali na wadau mbalimbali wa maswala ya usalama barabarani hatuna budi kushirikiana na wanajamii ili kutoa elimu ya usalama barabarani kwani zinahuitaji mkubwa wa kupata elimu hii na zinaguswa sana kwani wao ndo hupoteza watoto wao kutokana na tatizo hili,hadi nyakati nyingine hufikia hatua za kutaka kufunga barabara kwa sababu ya watoto wao hupatwa na ajili hizi wengine kupatwa na ulemavu na wengine kupoteza maisha.
Miundo mbinu pia inapaswa kurekebishwa na kuboreshwa zaidi bila kusahau kuweka matuta panapo stahili ili kupunguza mwendo kasi wa vyombo vya usafiri. Tunatoa rai kwa madereva wote wa vyombo vya moto kutii sheria za barabarani kwa vitendo ili tuweza kumaliza ajali hizi kabisa.
"Watoto Daraja Bora katika Jamii"
0 comments: